• HABARI MPYA

  Wednesday, June 23, 2021

  GWAMBINA FC YAPAMBANIA UHAI WAKE LIGI KUU TANZANIA BARA, YAJITUTUMIA KUCHAPA DODOMA JIJI 2-0 MISUNGWI

  TIMU ya Gwambina FC imeibuka na ushindi wa 2-0 dhidi ya Dodoma Jiji FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Gwambina, Misungwi mkoani Mwanza.
  Mabao ya Gwambina FC yote yamepatikana mapema kipindi cha kwanza na yamefungwa na mshambuliaji Paul Nonga dakika ya tisa na kiungo anayechezeshwa nafasi za ulinzi pia, Gustapha Simon dakika ya 45 na ushei.
  Kwa ushindi huo, Gwambina FC inafikisha pointi 34 baada ya kucheza mechi 32 na kupanda kwa nafasi moja hadi ya 16 ikiizidi tu wastani wa mabao Coastal Union ya Tanga.

  Dodoma Jiji FC yenyewe inabaki na pointi zake 42 za mechi 32 sasa katika nafasi ya nane, nayo ikizidiwa tu wastani wa mabao na zote, Tanzania Prisons ya Mbeya iliyohamishia maskani Sumbawanga mkoani Rukwa na KMC ya Kinondoni Jijini Dar es Salaam.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: GWAMBINA FC YAPAMBANIA UHAI WAKE LIGI KUU TANZANIA BARA, YAJITUTUMIA KUCHAPA DODOMA JIJI 2-0 MISUNGWI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top