• HABARI MPYA

  Wednesday, June 02, 2021

  AZAM FC YAMUONGEZEA MKATABA WA MIAKA MIWILI PRINCE DUBE MPUMELELO ATADUMU CHAMAZI HADI 2024

  KLABU ya Azam FC imeingia mkataba mpya wa miaka miwili zaidi na mshambuliaji wake wa kimataifa wa Zimbabwe, Prince Dube Mpumelelo, ambao utamfanya awe mali wa klabu huyo hadi mwaka 2024.
  "Dube ambaye tumemsajili msimu huu, amekuwa na kiwango bora kabisa hadi sasa akiwa ndiye kinara wa ufungaji bora kwenye Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) akiwa na mabao 14," amesema Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Abdulkarim Amin 'Popat'.
  Mbali na mabao hayo 14, kwa ujumla msimu huu, Dube amefunga mabao 17 kwenye mashindano yote, mengine matatu akitupia katika michuano ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC).


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AZAM FC YAMUONGEZEA MKATABA WA MIAKA MIWILI PRINCE DUBE MPUMELELO ATADUMU CHAMAZI HADI 2024 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top