• HABARI MPYA

  Monday, June 28, 2021

  UBELGIJI YAITUPA NJE URENO NA RONALDO WAO EURO 2020

  UBELGIJI wamefanikiwa kwenda Robo Fainali ya Euro 2020 baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya mabingwa watetezi, Ureno usiku huu Uwanja wa Olímpico Jijini Sevilla nchini Hispania.
  Pongezi kwa mfungaji ww bao hilo pekee, kiungo Thorgan Hazard dakika ya 42 akimalizia pasi ya mchezaji mwenzake wa Borussia Dortmund, beki Thomas Meunier.
  Sasa Ubelgiji watakutana na Italia Ijumaa baada ya kumfungisha virago Cristiano Ronaldo na wenzake katika Hatua ya 16 Bora tu.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: UBELGIJI YAITUPA NJE URENO NA RONALDO WAO EURO 2020 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top