• HABARI MPYA

  Saturday, June 19, 2021

  UJERUMANI YAZINDUKA NA KUICHAPA URENO YA RONALDO 4-2

  UJERUMANI imezinduka na kuichapa Ureno 4-2 katika mchezo wa Kundi F Euro 2020 leo Uwanja wa Allianz Arena Jijini Munich.
  Mabao ya Ujerumani yamefungwa na Rúben Dias dakika 35, Raphael Guerreiro dakika ya 39 wote wakijifunga, Kai Havertz dakika ya 51 na Robin Gosens dakika ya 60, wakati ya Ureno yamefungwa na Cristiano Ronaldo dakika 15 na Diogo Jota dakika ya 67.
  Ujerumani sasa ina pointi tatu sawa na Ureno, wakiwa nyuma ya Ufaransa inayoongoza kwa pointi zake nne na mbele ya Hungary yenye pointi moja baada ya mechi mbili mbili za mwanzo.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: UJERUMANI YAZINDUKA NA KUICHAPA URENO YA RONALDO 4-2 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top