• HABARI MPYA

  Sunday, June 20, 2021

  WALES YATINGA 16 BORA EURO 2020 LICHA YA KUCHAPWA 1-0 NA ITALIA

  ITALIA imekamilisha mechi zake za Kundi A Euro 2020 kwa ushindi wa 1-0 dhidi ya Wales usiku huu, bao pekee la kiungo wa Atalanta,Matteo Pessina Uwanja wa Olimpico Jijini Roma.
  Mechi nyingine ya kundi hilo, Uswisi imeichapa Uturuki 3-1 Uwanja wa Olimpiya mjini Baku nchini Azerbaijan.
  Mabao ya Uswisi yamefungwa na Haris Seferović dakika ya sita na Xherdan Shaqiri mawili dakika ya 26 na 68, wakati la Uturuki limefungwa na İrfan Can Kahveci dakika ya 62.


  Italia inamaliza na pointi tisa, ikifuatiwa na Wales yenye pointi nne na zote zinakwenda 16 Bora, wakati Uswisi iliyomaliza na pointi nne pia ikiziwa wastani wa mabao na Uturuki bila pointi zinaishia hapa.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: WALES YATINGA 16 BORA EURO 2020 LICHA YA KUCHAPWA 1-0 NA ITALIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top