• HABARI MPYA

  Thursday, June 24, 2021

  RUVU SHOOTING YALAZIMISHWA SARE YA KUFUNGANA BAO 1-1 NA POLISI TANZANIA LEO UWANJA WA MABATINI MECHI YA LIGI KUU

  RUVU Shooting imelazimishwa sare ya 1-1 na Polisi Tanzania katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara leo Uwanja wa Mabatini, Mlandizi mkoani Pwani.
  David Ulomi alianza kuifungia Ruvu Shooting dakika ya 34, kabla ya Tariq Seif kuisawazishia Polisi Tanzania dakika ya 58.
  Kwa ushindi huo, Polisi Tanzania imefikisha pointi 42 baada ya kucheza mechi 32 na kusogea nafasi ya saba, wakati Ruvu Shooting inayofikisha pointi 38 za mechi 32 pia inasonga nafasi ya 10.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: RUVU SHOOTING YALAZIMISHWA SARE YA KUFUNGANA BAO 1-1 NA POLISI TANZANIA LEO UWANJA WA MABATINI MECHI YA LIGI KUU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top