• HABARI MPYA

  Tuesday, June 15, 2021

  POLAND YAANZA VIBAYA EURO 2020, YAPIGWA 2-1 NA SLOVAKIA

  TIMU ya taifa ya Poland imeanza vibaya Euro 2020 baada ya kuchapwa mabao 2-1 na Slovakia katika mchezo wa Kundi E usiku wa jana Uwanja wa Saint-Petersburg Jijini St. Petersburg, Urusi.
  Kipa Wojciech Szczęsny wa Juventus alijifunga dakika ya 18 kuipatia Slovakia bao la kwanza, kabla ya beki wa Inter Milan Milan Skriniar kufunga la pili dakika ya 69, wakati bao la Poland lilifungwa na kiungo wa Torino Karol Linetty dakika ya 46.
  Nayo Scotland ilichapwa 2-0 na Jamhuri ya Czech Republic, mabao ya mshambuliaji wa Bayer Leverkusen, Patrik Schick dakika ya 42 na 52 katika mchezo wa Kundi D Uwanja wa Venue Hampden Park Jijini Glasgow.


  Hispania ikalazimishwa sare ya bila kufungana na Sweden katika mchezo mwingine wa Kundi E Uwanja wa Olimpico de Sevilla Jijini Sevilla.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: POLAND YAANZA VIBAYA EURO 2020, YAPIGWA 2-1 NA SLOVAKIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top