• HABARI MPYA

  Thursday, June 17, 2021

  MTIBWA SUGAR YAICHAPA SIMBA 3-1, KUKUTANA NA YANGA FAINALI LIGI YA VIJANA U20 JUMAMOSI CHAMAZI

   MABINGWA watetezi, Mtibwa Sugar wamefanikiwa kwenda Fainali ya Ligi Kuu ya Vijana chini ya umri wa miaka 20 baada ya ushindi wa 3-1 dhidi ya Simba SC Uwanja wa Azam Complex, Chamazi nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.
  Mabao ya Mtibwa Sugar yamefungwa na Joseph Mkelle dakika ya 14 na Omary Marungu dakika ya 54 kwa penalti na 80, wakati bao pekee la Simba limefungwa na Kassim Omar dakika ya 68.
  Sasa Mtibwa Sugar itakutana na Yanga katika Fainali Jumamosi, wakati Simba itamenyana na Azam FC katika mechi ya kusaka mshindi wa tatu hapo hapo Azam Complex.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MTIBWA SUGAR YAICHAPA SIMBA 3-1, KUKUTANA NA YANGA FAINALI LIGI YA VIJANA U20 JUMAMOSI CHAMAZI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top