• HABARI MPYA

  Wednesday, June 23, 2021

  RAHEEM STERLING AIPELEKA ENGLAND 16 BORA EURO 2020

  ENGLAND imefanikiwa kwenda Hatua ya 16 Bora baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya Jamhuri ya Czech usiku wa jana Uwanja wa Wembley Jijini London.
  Katika mchezo huo wa Kundi D, bao pekee la England limefungwa na nyota wa Manchester City, Raheem Sterling dakika ya 12 na kwa ushindi huo Three Lions inamaliza kileleni kwa pionti zake saba, mbele ya Croatia yenye pointi nne na zote zinafuzu 16 Bora.
  Bahati mbaya kwao Czech wamezidiwa wastani wa mabao tu na Croatia, kwani nao wamemaliza na pointi tatu, wakati Scotland imeshika mkia kwa pointi yake moja.

  Mechi nyingine ya mwisho ya kundi hilo jana, iliichapa Scotland 3-1 Uwanja wa Hampden Park Jijini Glasgow. Mabao ya Croatia yalifungwa na Nikola Vlasic dakika ya 17, Luka Modric dakika ya 62 na Ivan Perisic dakika ya 77, wakati la Scotland alifunga Callum William McGregor dakika ya 42.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: RAHEEM STERLING AIPELEKA ENGLAND 16 BORA EURO 2020 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top