• HABARI MPYA

  Thursday, June 17, 2021

  FEISAL APIGA MBILI YANGA SC YAICHAPA RUVU SHOOTING 3-2 MECHI YA LIGI KUU LEO DAR

   VIGOGO, Yanga SC wameibuka na ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Ruvu Shooting katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara usiku huu Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
  Mabao ya Yanga leo yamefungwa na kiungo Feisal Salum Abdallah mawili, dakika ya 23 na 32 na Mrundi, Said Ntibanzokiza dakika ya 80, wakati ya Ruvu Shooting yamefungwa na Emmanuel Martin dakika ya 70 na David Richard dakika ya 82.
  Kwa ushindi huo, Yanga SC inafikisha pointi 64 baada ya kucheza mechi 30, ingawa inabaki nafasi ya pili ikizidiwa pointi tatu na mabingwa watetezi, Simba SC ambao pia wana mechi tatu mkononi.
  Ruvu Shooting yenyewe inabaki na pointi zake 37 za mechi 31 sasa katika nafasi ya 10.


  Mechi nyingine za Ligi Kuu leo, Mtibwa Sugar imeichapa Mwadui FC 3-1 Uwanja wa Mwadui Complex, Kishapu mkoani Shinyanga na Dodoma Jiji FC wameilaza KMC 1-0 Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: FEISAL APIGA MBILI YANGA SC YAICHAPA RUVU SHOOTING 3-2 MECHI YA LIGI KUU LEO DAR Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top