• HABARI MPYA

  Thursday, June 03, 2021

  BOCCO APIGA MBILI SIMBA SC YAITANDIKA RUVU SHOOTING 3-0 CCM KIRUMBA NA KUWATIMULIA VUMBI YANGA SC

   MABINGWA watetezi, Simba SC wameendeleza wimbi la ushindi katika Ligi Kuu ya Tanzania Bara baada ya kuichapa Ruvu Shooting 3-0 Uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza.
  Nahodha wa Simba SC, John Raphael Bocco amefunga mabao mawili, la kwanza dakika ya 18 akimalizia pasi ya kiungo wa kimataifa wa Msumbiji na la tatu dakika ya 88 kwa penalti baada ya kipa wa Ruvu, Abdallah Rashid kumuangusha winga Mghana, Bernard Morrison kwenye boksi.
  Morrison, mchezaji wa zamani wa mahasimu, Yanga SC ndiye aliyemsetia mshambuliaji Mkongo, Chris Kope Mugalu kufunga bao la pili dakika ya 62.

  Kwa ushindi huo Simba SC imefikisha pointi 67 baada ya kucheza mechi 27 na kuendelea kuongoza Ligi Kuu kwa pointi sita zaidi ya Yanga ambao pia wamecheza mechi mbili zaidi. 
  Ruvu Shooting ilimaliza pungufu mechi hiyo baada ya wachezaji wake wawili kutolewa kwa kadi nyekundu, beki wake, Juma Said Nyosso dakika ya 72 na kipa Abdallah Rashid dakika ya 87.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: BOCCO APIGA MBILI SIMBA SC YAITANDIKA RUVU SHOOTING 3-0 CCM KIRUMBA NA KUWATIMULIA VUMBI YANGA SC Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top