• HABARI MPYA

  Wednesday, June 09, 2021

  MCHAMBUZI WA SOKA, OSCAR OSCAR ACHUKUA FOMU KUWANIA URAIS WA TFF KATIKA UCHAGUZI ULIOPANGWA KUFANYIKA AGOSTI 7 JIJINI TANGA

   

  MCHAMBUZI wa soka, Oscar. Oscar amejitokeza kuwania Urais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) katika uchaguzi uliopangwa kufanyika Agosti 7 mwaka huu Jijini Tanga.
  Pamoja na Oscar, mwingine aliyechukua fomu leo zinazotolewa kwa gharama ya Sh. 500,000 ni Deogratius Mutungi ambao wanafanya idadi ya wagombea Urais kufika watano, wengine Evans Mgeusa, Zahor Mohamed Hajji na Rais wa sasa, Wallace John Karia.
  Zoezi la uchukuaji fomu linatarajiwa kuendelea hadi Jumamosi Saa 10:00 jioni makao makuu ya TFF, Uwanja wa Karume Jijini Dar es Salaam au kupitia tovuti ya shirikisho hilo.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MCHAMBUZI WA SOKA, OSCAR OSCAR ACHUKUA FOMU KUWANIA URAIS WA TFF KATIKA UCHAGUZI ULIOPANGWA KUFANYIKA AGOSTI 7 JIJINI TANGA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top