• HABARI MPYA

  Monday, June 14, 2021

  SIMBA SC NAYO YATINGA NUSU FAINALI LIGI YA VIJANA U20 BAADA YA USHINDI WA 1-0 DHIDI YA JKT TANZANIA AZAM COMPLEX

   TIMU ya Simba SC imefanikiwa kutinga Nusu Fainali ya Ligi Kuu ya Vijana chini ya umri wa miaka 20 baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya JKT Tanzania katika mchezo wa Kundi A usiku huu Uwanja wa Azam Complex, Chamazi nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.
  Simba inafikisha pointi saba baada ya mechi zote tatu za kundi hilo, ikishinda mbili zote 1-0, nyingine dhidi ya Mwadui FC na sare ya bila kufungana na watani wa jadi, Yanga SC.
  Simba inayofundishwa na Nico Kiondo inamaliza na pointi saba katika nafasi ya pili ikizidiwa tu wastani wa mabao na Yanga.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA SC NAYO YATINGA NUSU FAINALI LIGI YA VIJANA U20 BAADA YA USHINDI WA 1-0 DHIDI YA JKT TANZANIA AZAM COMPLEX Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top