• HABARI MPYA

  Tuesday, June 22, 2021

  AERGENTINA YANG'ARA COPA AMERICA, YAICHAPA PARAGUAY 1-0

  BAO pekee la kiungo wa Sevilla, Alejandro Darío Gómez dakika ya 10 jana limeipa Argentina ushindi wa 1-0 dhidi ya Paraguay katika mchezo wa Kundi A michuano ya Copa America Uwanja wa Taifa wa Brasília nchini Brazil.
  Argentina inafikisha pointi saba na kuendelea kuongoza kundi hilo kwa pointi mbili zaidi ya Chile inayofuatia baada ya wote kucheza mechi tatu.
  Kwa upande wao Paraguay wanabaki nafasi ya tatu na pointi zao tatu, wakifuatiwa na Uruguay pointi moja na Bolivia wanashika mkia hawana pointi.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AERGENTINA YANG'ARA COPA AMERICA, YAICHAPA PARAGUAY 1-0 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top