• HABARI MPYA

    Thursday, June 24, 2021

    KAMATI YA MAADILI YA TFF YAMFUTIA ADHABU YA KUMFUNGIA MWAKALEBELA MIAKA MITANO KWA TUHUMA ZA UCHOCHEZI

     KAMATI ya Maadili ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) imemfutia adhabu ya kufungiwa miaka mitano kutojisjighulisha na soka pamoja na faini ya Sh. Milioni 7 aliyopewa na Aprili 2, mwaka huu na Kamati hiyo.
    Mwakalebela alitozwa faini ya Sh Milioni 5 baada ya kutiwa hatiani kwa kutoa maneno ya uchochezi kwa nia ya kuchochea mashabiki, wanachama na wapenzi wa Yanga dhidi ya vyombo vinavyosimamia mpira wa miguu nchini.
    Uamuzi huo ulitolewa na Kamati ya Maadili ya TFF kwa kuzingatia kifungu cha 73(4) cha kanuni za maadili za TFF toleo la 2013.


    Mwakalebela alilalamikiwa kuwa Februari 19 mwaka huu aliitisha mkutano na Waandishi wa Habari na kudai kuwa TFF, Bodi ya Ligi Kuu Tazania Bara (TPLB) na Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa ligi hiyo zinaihujumu Yanga, madai ambayo alishindwa kuthibitisha mbele ya kamati.
    Katika shtaka la pili, Mwakalebela alilalamikiwa kwa kutoa taarifa za uongo Oktoba 1, 2020 baada ya kuitisha mkutano na kudai kuwa anao mkataba kati ya mchezaji Bernard Morrison na klabu ya Simba na kuuonyesha kwa Waandishi wa Habari huku akijua ni uongo na kitendo hicho ni kinyume na sheria.
    Kamati ya maadili ilimtia hatiani katika shtaka hilo na kumpa onyo la kutotenda kosa hilo tena kwa musa wa miaka mitano pamoja na kumtoza faini ya Sh Milioni 2 na adhabu hizo ni kwa mujibu wa kifungu cha 6(1) (b) na 6(1) (c) cha kanuni za TFF toleo la 2013.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: KAMATI YA MAADILI YA TFF YAMFUTIA ADHABU YA KUMFUNGIA MWAKALEBELA MIAKA MITANO KWA TUHUMA ZA UCHOCHEZI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top