• HABARI MPYA

  Thursday, June 17, 2021

  ITALIA YASONGA MBELE EURO 2020 BAADA YA KUICHAPA USWISI 3-0

   WENYEJI, Italia wameibuka na ushindi wa 3-0 dhidi ya Uswisi katika mchezo wa Kundi A Euro 2020 usiku wa Jumatano Uwanja wa Olimpico Jijini Roma.
  Mabao ya Italia yamefungwa na Manuel Locatelli mawili, dakika ya 26 na 52 na Ciro Immobile dakika ya 89.
  Kwa matokeo hayo, Azzuri inafikisha pointi sita baada ya mechi mbili na kuwa timu ya kwanza kwenda Hatua ya 16 Bora, ikiizidi pointi mbili Wales inayofuatia mbele ya Usiwsi yenye pointi moja, wakati Uturuki ambayo haina pointi inashika mkia.
  Mechi nyingine ya kundi hilo, Wales imeichapa Uturuki 2-0, mabao ya  Aaron Ramsey dakika ya 42 na Connor Roberts dakika ya 90 na ushei Uwanja wa Bakı Olimpiya Jijini Baku.


  Aidha, katika mchezo wa Kundi B, Urusi imeichapa Finland 1-0, bao pekee la Aleksey Miranchuk dakika ya 45 Uwanja wa Saint-Petersburg.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: ITALIA YASONGA MBELE EURO 2020 BAADA YA KUICHAPA USWISI 3-0 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top