• HABARI MPYA

  Tuesday, June 29, 2021

  MBAPPE AKOSA PENALTI YA MWISHO UFARANSA YATUPWA NJE EURO 2020

  USWISI imetinga Robo Fainali ya Euro 2020 baada ya ushindi wa penalti 5-4 kufuatia sare ya kufungana mabao 3-3 ndani ya dakika 120 usiku huu Uwanja wa Taifa wa Bucharest nchini Romania.
  Mabao ya Uswis yamefungwa na Haris Seferović dakika ya 15 na 81 na Mario Gavranović dakika ya 90, wakati ya Ufaransa yamefungwa na Karim Benzema dakika ya 57 na 59 na Paul Pogba dakika ya 75.
  Na katika mikwaju ya penati Mario Gavranović, Fabian Schär, Manuel Akanji, Ruben Martínez na Admir Mehmedi waliifungia Uswisi, wakati Pogba, Olivier Giroud, Marcus Thuram na Presnel Kimpembe walifunga za Ufaransa, kabla ya Kylian Mbappé kukosa ya mwisho iliyopanguliwa na kipa Yann Sommer.
  Kwa matokeo hayo, Uswisi itakutana na Hispania katika Robo Fainali Ijumaa.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MBAPPE AKOSA PENALTI YA MWISHO UFARANSA YATUPWA NJE EURO 2020 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top