• HABARI MPYA

  Wednesday, June 09, 2021

  GIROUD APIGA MBILI UFARANSA YAICHAPA BULGARIA 3-0

  UFARANSA jana imeibuka na ushindi wa 3-0 dhidi ya Bulgaria katika mchezo wa mwisho wa kujiandaa na Euro 2020 mabao ya Antoine Griezmann dakika ya 29 na Olivier Giroud, mawili dakika za 83 na 90.
  Les Bleus walipata pigo kwenye mchezo huo kufuatia mshambuliaji wake mkongwe, Karim Benzema kuumia goti.
  Ufaransa waliopangwa Kundi F, watafungua dimba na Ujerumani Juni 15 Uwanja wa Allianz Arena Jijini Munch, kabla ya kumenyana na Hungary Juni 19 na kukamilisha mechi zake za kundi hilo kwa kucheza na Ureno Juni 23 mechi hizo mbili zikichezwa Uwanja wa Puskas Arena Jijini Budapest.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: GIROUD APIGA MBILI UFARANSA YAICHAPA BULGARIA 3-0 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top