• HABARI MPYA

  Sunday, June 20, 2021

  HISPANIA YALAZIMISHWA SARE NA POLAND 1-1 SEVILLA

   TIMU ya taifa ya Hispania imelazimishwa sare ya 1-1 na Poland katika mchezo wa Kundi E Euro 2020 usiku huu Uwanja wa Olímpico Jijini Sevilla.
  Morata alianza kuifungia Hispania dakika ya 25 akimalizia pasi ya Gerard Moreno, kabla ya Robert Lewandowski dakika ya 54.
  Hispania ilipoteza nafasi ya kupata ushindi baada ya Moreno kukosa penalti kipindi cha pili kwa kugongesha mwamba na mpira kurudi uwanjani, hata Morata alipojaribu kuunganisha mpira ukaenda nje.


  Sare hiyo ya pili na mfululizo kwa Hispania inawafanya wafikishe pointi mbili katika nafasi ya tatu kundini, nyuma ya Sweden pointi nne na Slovakia tatu, wakati Poland inaokota pointi ya kwanza leo baada ya mechi mbili, hivyo kuendelea kushika mkia.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: HISPANIA YALAZIMISHWA SARE NA POLAND 1-1 SEVILLA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top