• HABARI MPYA

  Wednesday, June 30, 2021

  MESSI BADO BAO MOJA TU AMFIKIE MAREHEMU MARADONA ARGENTINA

  NYOTA wa Barcelona, Lionel Messia juzi amefunga mabao mawili kuiwezesha Argentina kuichapa Bolivia 4-1 katika mchezo wa mwisho wa Kundi A Copa America huko Brazil na kubakiuza bao moja kumfikia gwiji wa Argentina, Diego Maradona.
  Messi mwenye umri wa miaka 34 sasa, amefikisha mabao 31 katika mechi 148, wakati marehemu Maradona alifunga 32 katika mechi 87, zikiwemo za ushindi wa Kombe la Dunia 1986, wakati Messi bado hajashinda taji na timu yake hiyo ya taifa.
  Messi pia ameweka rekodi ya mchezaji aliyeichezea mechi nyingi zaidi timu ya taifa ya Argentina, akimpiku beki mstaafu, Javier Mascherano.  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MESSI BADO BAO MOJA TU AMFIKIE MAREHEMU MARADONA ARGENTINA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top