• HABARI MPYA

  Thursday, June 10, 2021

  MBUNGE TARIMBA ABBAS NA NAHODHA WA ZAMANI WA TAIFA STARS, ALLY MAYAY WACHUKUA FOMU KUGOMBEA URAIS WA TFF DHIDI WALLACE KARIA


   MBUNGE wa jimbo la Kinondoni (CCM), Tarimba Gullam Abbas amechukua fomu kuwania Urais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) katika uchaguzi uliopangwa kufanyika Agosti 7 Jijini Tanga.
  Pamoja na Tarimba, Rais wa zamani wa klabu ya Yanga, wengine waliochukua fomu leo ni Nahodha na kiungo wa zamani wa klabu hiyo na timu ya taifa, Ally Mayay Tembele.
  Wawili hao wanafanya idadi ya jumla ya wagombea saba wa nafasi ya Urais pekee, akiwemo Rais anayemaliza muda wake, Wallace John Karia anayeomba tena ridhaa, Oscar Oscar, Deogratius Mutungi, Evans Mgeusa na Zahor Mohammed Hajji.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MBUNGE TARIMBA ABBAS NA NAHODHA WA ZAMANI WA TAIFA STARS, ALLY MAYAY WACHUKUA FOMU KUGOMBEA URAIS WA TFF DHIDI WALLACE KARIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top