• HABARI MPYA

  Thursday, June 03, 2021

  KOCHA MAARUFU NCHINI, JAMHURI KIHWELO 'JULIO' AENGULIWA KUWANIA UENYEKITI WA CHAMA CHA MAKOCHA TANZANIA, MENEJA WA SAMATTA APETA


  KOCHA maarufu nchini na mchezaji wa zamani wa timu ya taifa, Jamhuri Mussa Kihwelo 'Julio' ameenguliwa kwenye Uchaguzi wa Chama cha Makocha Tanzania (TAFCA) kwa madai hakuhudhuria usaili uliofanyika juzi.
  Taarifa ya Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) leo imesema pamoja na Julio aliyeomba kuwania nafasi ya Uenyekiti, mgombea mwingine wa nafasi hiyo, kipa wa zamani wa Taifa Stars, Ivo Philip Mapunda pia ameenguliwa kwa sababu hakuhudhuria usaili huo.
  Aliyepitishwa ni mchezaji mwingine wa zamani wa Taifa Stars, Leopold Mukebezi 'Tasso' pekee kuwania nafasi hiyo, wakati nafasi ya Makamu Mwenyekiti amepitishwa Jamal Kisongo pekee, Meneja wa zamani wa Nahodha wa Taifa Stars, Mbwana Ally Samatta anayechezea Fenerbahce ya Uturuki kwa sasa.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KOCHA MAARUFU NCHINI, JAMHURI KIHWELO 'JULIO' AENGULIWA KUWANIA UENYEKITI WA CHAMA CHA MAKOCHA TANZANIA, MENEJA WA SAMATTA APETA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top