• HABARI MPYA

  Friday, June 18, 2021

  METACHA MNATA AWAOMBA RADHI YANGA SC KWA KUWATUKANA MASHABIKI JANA BAADA YA MECHI NA RUVU DAR

   KIPA wa Yanga SC, Metacha Boniphace Mnata ameomba radhi kwa kwa kitendo chake cha kuwatukana mashabiki jana Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.
  "Kwa niaba ya Familia yangu, Management yangu na mimi mwenyewe napenda kuchukua fursa hii kuomba msamaha kwa Viongozi wa Klabu yangu ya Yanga SC, Wachezaji wenzangu, Benchi la Ufundi, Mashabiki wa Klabu ya Yanga, Mamlaka za soka nchini na wadau wote soka ambao wamekwazika kwa kwa kitendo nilichokifanya jana,".
  "Nikiri hakikuwa kitendo cha kiungwana hivyo najutia makosa niliyoyafanya. Mimi kama mchezaji wa Yanga na Timu ya Taifa napaswa kuwa mfano mzuri siku zote mbele za watoto na  wanaotamani kuwa kama mimi na watu ambao aidha walikuwepo kiwanjani au waliona mechi kupitia Televisheni majumbani kwao,".
  "Natambua mchango na umuhimu wa mashabiki kwangu binafsi na kwa Klabu, hivyo kitendo kile hakikupaswa kutokea. Natanguliza Shukrani 🙏
  #DaimaMbeleNyumaMwiko," ameandika Mnata katika ukurasa wake wa Instagram.


  Yanga jana ilimsimamisha Mnata kwa muda usiojulikana kutokana na utovu wa nidhamu.
  Mashabiki wa Yanga walikerwa na kitendo cha Mnata kuruhusu mabao mawili rahisi timu ikishinda 3-2 dhidi ya Ruvu Shooting katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara usiku wa jana Uwanja wa Benjamin Mkapa.
  Na wakati anatolewa uwanjani kwa msaada wa askari Polisi kumuepusha na mikono ya mashabiki wenye hasira waliokuwa wanamtolewa maneno makali na kumtupia chupa, kipa huyo akawaonyesha ishara ya kuwatusi.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: METACHA MNATA AWAOMBA RADHI YANGA SC KWA KUWATUKANA MASHABIKI JANA BAADA YA MECHI NA RUVU DAR Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top