• HABARI MPYA

  Saturday, June 05, 2021

  WATANI WA JADI SIMBA NA YANGA KUFUNGUA DIMBA KATIKA LIGI KUU YA VIJANA U20 JUNI 10 AZAM COMPLEX

  WAPINZANI wa jadi, Simba na Yanga wamepangwa kundi moja , A katika Ligi Kuu ya Vijana chini ya umri wa miaka 20 inayotarajiwa kuanza Juni 10 Uwanja wa Azam Complex, Chamazi nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.
  Na watani hao wa jadi ndiyo watakaofungua dimba siku hiyo Saa 3:00 usiku, mchezo ambao utatanguliwa na mechi nyingine ya kundi hilo baina ya JKT Tanzania na Mwadui FC Saa 1:00 usiku.
  Mechi za kwanza za Kundi B zitafuatia Juni 11, Tanzania Prisons na Kagera Sugar Saa 1:00 na Azam FC dhidi ya mabingwa watetezi, Mtibwa Sugar Saa 3:00 usiku.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: WATANI WA JADI SIMBA NA YANGA KUFUNGUA DIMBA KATIKA LIGI KUU YA VIJANA U20 JUNI 10 AZAM COMPLEX Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top