• HABARI MPYA

  Monday, June 07, 2021

  AZAM FC YABEBA TUZO ZOTE ZA LIGI KUU MWEZI MEI KUANZIA MCHEZAJI, KOCHA HADI MENEJA BORA WA UWANJA

   BODI ya Ligi Tanzania (TPLB) imetaja vinara wa Ligi Kuu Tanzania Bara mwezi Mei, mwaka huu na Azam FC imebeba zote.
  Mzambia George Lwandamina ametwaa tuzo ya Kocha Bora, mshambuliaji Mzimbabwe, Prince Dube Mpumelelo amebeba tuzo ya Mchezaji Bora, wakati Sikitu Kilakala amekuwa Meneja Bora wa Uwanja kwa mwezi huo.
  Wakati Dube amewashinda Erick Mwijage wa Kagera Sugar na kipa wa Yanga SC, Metacha Mnata alioingia nao fainali, Lwandamina amewabwaga Mkenya Francis Baraza wa Kagera Sugar na Abdallah Mohamed wa JKT Tanzania.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AZAM FC YABEBA TUZO ZOTE ZA LIGI KUU MWEZI MEI KUANZIA MCHEZAJI, KOCHA HADI MENEJA BORA WA UWANJA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top