• HABARI MPYA

  Friday, June 25, 2021

  CHIPUKIZI MWENYE KIPAJI MTANZANIA, KELVIN JOHN AJIUNGA NA TIMU YA ZAMANI YA SAMATTA, GENK HADI MWAKA 2024

   MSHAMBULIAJI chipukizi wa kimataifa wa Tanzania, Kelvin John Pius mwenye umri wa miaka 18 amejiunga  klabu ya KRC Genk ya Ubelgiji baada ya kusaini utakaomalizika mwaka 2024.
  Taarifa rasmi ya Genk leo imemshukuru mchezaji wake wa zamani, Mtanzania pia, Mbwana Ally Samatta kwa kuwasaidia kuinasa saini ya kinda huyo mwenye kipaji kutoka akademi ya Brook House Collage ya England aliyojiunga nayo mwaka 2019 baada ya kung'ara kwenye Fainali za Vijana Afrika chini ya umri wa miaka 17.
  Samatta, Nahodha wa Taifa Stars mwenye umri wa miaka 28 sasa, alipita Genk kwa miaka minne kuanzia 2016 kabla ya kwenda Aston Villa ya England mwaka 2020 ambayo baada ya miezi kadhaa ilimtoa kwa mkopo Fenerbahce ya Uturuki.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: CHIPUKIZI MWENYE KIPAJI MTANZANIA, KELVIN JOHN AJIUNGA NA TIMU YA ZAMANI YA SAMATTA, GENK HADI MWAKA 2024 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top