• HABARI MPYA

  Thursday, June 24, 2021

  BRAZIL YATINGA ROBO FAINALI BAADA YA KUICHAPA COLOMBIA 2-1

  WENYEJI, Brazil wamefuzu Robo Fainali ya Copa America baada ya ushindi wa 2-1 dhidi ya Colombia katika mchezo wa Kundi B usiku wa kuamkia leo Uwanja wa Nilton Santos Jijini Rio de Janeiro.
  Mabao ya Brazil yamefungwa na Roberto Firmino dakika ya 78 akimalizia pasi ya Renan Lodi na Casemiro dakika ya 90 na ushei akimalizoa pasi ya Neymar, wakati la Colombia limefungwa na Luis Díaz dakika ya 10 akimalizia pasi ya J. Cuadrado.
  Brazil inafikisha pointi tisa baada ya kucheza mechi tatu ma kuendelea kuongoza kundi hilo, ikifuatiwa na Colombia yenye pointi nne za mechi nne, Peru pointi nne pia, Ecuador na Venezuela pointi mbili kila timu baada ya kucheza mechi tatu wote pia.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: BRAZIL YATINGA ROBO FAINALI BAADA YA KUICHAPA COLOMBIA 2-1 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top