• HABARI MPYA

  Monday, June 21, 2021

  UHOLANZI YATINGA 16 BORA EURO 2020 BAADA YA KUIPIGA MACEDONIA 3-0

  UHOLANZI wamefanikiwa kwenda Hatua ya 16 Bora Euro 2020 baa ya ushindi wa 3-0 Macedonia Kaskazini kwenye mchezo wa Kundi C leo Uwanja wa Johan Cruijff Arena Jijini Amsterdam.
  Mabao ya Uholanzi yamefungwa na Memphis Depay dakika ya 24 na Georginio Wijnaldum mawili dakika ya 51 na 58.
  Mechi nyingine ya mwisho ya Kundi C, Auatria imeilaza Ukraine 1-0, bao pekee la Christoph Baumgartner dakika ya 21 Uwanja wa Taifa wa Bucharest nchini Romania.


  Uholanzi imemaliza kileleni kwa pointi tisa, ikifuatiwa na Ukraine pointi sita na zote zinafuzu 16 Bora zikizipiku Austria iliyomaliza na pointi tatu, wakati Macedonia Kaskazini haina pointi imeshika mkia.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: UHOLANZI YATINGA 16 BORA EURO 2020 BAADA YA KUIPIGA MACEDONIA 3-0 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top