• HABARI MPYA

  Saturday, May 28, 2022

  FEI TOTO AIPELEKA YANGA FAINALI ASFC, SIMBA YALALA 1-0


  VIGOGO, Yanga SC wamefanikiwa kwenda Fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya mahasimu, Simba SC jioni ya leo Uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza.
  Pongezi kwa mfungaji wa bao hilo pekee, kiungo Mzanzibari, Feisal Salum Abdallah ‘Fei Toto’ dakika ya 25 akimalizia pasi ya kiungo Mganda, Khalid Aucho.
  Sasa Yanga itakutana na mshindi kati ya Azam FC na Coastal Union zitakazomenyana kesho Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Jijini Arusha katika Fainali Julai 2 huko huko Arusha.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: FEI TOTO AIPELEKA YANGA FAINALI ASFC, SIMBA YALALA 1-0 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top