• HABARI MPYA

  Thursday, June 10, 2021

  BRUNO APIGA MBILI, RONALDO MOJA URENO YAICHAPA ISRAEL 4-0

  KATIKA kujiandaa na Fainali za Euro 2020, Ureno jana iliichapa Israel 4-0 katika mchezo wa kirafiki Uwanja wa Jose Alvalade Jijini Lisbon.
  Mabao ya Ureno yalifungwa Bruno Fernandes mawili dakika ya 42 na 90 na ushei, Cristiano Ronaldo dakika ya 44 na Joao Cancelo dakika ya 86.
  Ureno inatarajiwa kutupa kete yake ya kwanza katika mchezo wa Kundi F Euro 2020 dhidi ya Hungary Jumanne ijayo Uwanja wa Puskas Arena Jijini Budapest kuanzia Saa 1:00 usiku kabla ya kumenyama na Ujerumani Juni 19 na kukamilisha mechiza kundi hilo kwa kuwavaa Ufaransa Juni 23.


  Fainali za Euro 2020 zinaanza kesho kwa mchezo kati ya Uturuki na Italia Saa 4:00 usiku Uwanja wa Olimpico Jijini Roma.
  Michuano hiyo iliyokuwa ifanyike Juni 12 hadi Julai 12 mwaka jana na kusogezwa mbele kuanzia kesho hadi Julai 11 kutokana na COVID 19 – itafanyika katika Majiji 11 ya nchi 11 tofauti za Ulaya kwa jina lile lile la "UEFA Euro 2020.
  Aliyekuwa Rais wa UEFA, Michel Platini ameamua ifanyike katika nchi tofauti badala ya nchi moja, au mbili pekee kama ilivyozoeleka ikiwa ni shamrashamra za kusherehekea miaka 60 ya michuano hiyo.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: BRUNO APIGA MBILI, RONALDO MOJA URENO YAICHAPA ISRAEL 4-0 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top