• HABARI MPYA

  Saturday, June 26, 2021

  SIMON MSUVA ACHEZA KIPINDI KIMOJA WYDAD YALAZIMISHWA SARE NA KAIZER CHIEFS JOHANNESBURG NA KUTOLEWA LIGI YA MABINGWA AFRIKA

   KIUNGO mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Simon Happygod Msuva amecheza kipindi kimoja leo timu yake, Wydad Athletic ya Morocco ikilazimishwa sare ya 0-0 na wenyeji, Kaizer Chiefs katika mchezo wa marudiano wa Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika Uwanja wa FNB Jijiji Johannesburg, Afrika Kusini.
  Msuva alimpisha kiungo Mlibya, Muaid Ellafi  kipindi cha pili na kwa sare hiyo, Kaizer Chiefs wanakwenda Fainali kufuatia ushindi wa 1-0 kwenye mchezo wa kwanza Jijini Casablanca nchini Morocco Jumamosi iliyopita.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMON MSUVA ACHEZA KIPINDI KIMOJA WYDAD YALAZIMISHWA SARE NA KAIZER CHIEFS JOHANNESBURG NA KUTOLEWA LIGI YA MABINGWA AFRIKA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top