• HABARI MPYA

  Tuesday, June 22, 2021

  YUSSUF POULSEN AIPELEKA DENMARK 16 BORA EURO 2020

  MSHAMBULIAJI mwenye asili ya Tanzania, Yussuf Poulsen jana amefunga bao Denmark ikiibuka na ushindi wa 4-1 dhidi ya Urusi katika mchezo wa Kundi B jana Uwanja wa Parken Jijini Copenhagen na kutinga Hatua ya 16 Bora Euro 2020.
  Yussuf Poulsen alifunga bao lake dakika ya 59, wakati mabao mengine ya Denmark yamefungwa na Mikkel Damsgaard dakika ya 38, Andreas Christensen dakika ya 79 na Joakim Mæhle dakika ya 82 na bao pekee la urusi lilifungwa kwa penalti na Artem Dzyuba dakika ya 70.
  Mechi nyingine ya kundi hilo, Ubelgiji iliichapa Finland 2-0, mabao ya Lukáš. Hrádecký aliyejifunga dakika ya 74 na Romelu Lukaku dakika ya 81 Uwanja wa Saint-Petersburg Jijini St. Petersburg nchini Urusi.


  Ubelgiji imeongoza kundi kwa pointi zake tisa, ikifuatiwa na Denmark yenye pointi tatu na zote zinafuzu 16 Bora zikizipiku Finland na Urusi zilizomaliza na pointi tatu pia kila mlja, lakini zimediwa wastani wa mabao. 


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YUSSUF POULSEN AIPELEKA DENMARK 16 BORA EURO 2020 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top