• HABARI MPYA

  Saturday, June 19, 2021

  ARGENTINA YAPATA USHINDI WA KWANZA COPA AMERICA

  ARGENTINA imepata ushindi wa kwanza katika Copa America baada ya kuichapa 1-0 Uruguay katika mchezo wa Kudi A usiku wa kuamkia leo Uwanja wa Taifa wa Brasilia, Distrito Federal.
  Pongezi kwa mfungaji wa bao hilo pekee, kiungo wa Real Betis Guido Rodríguez dakika ya 13 akimalizia pasi ya Nahodha na nyota mwenzake wa La Liga, Lionel Messi wa Barcelona.
  Sasa Argentina ina pointi nne baada ya mechi mbili kufuatia sare ya 1-1 na Chile kwenye mchezo wa kwanza, wakati Uruguay ilikuwa inacheza mechi ya kwanza jana.
  Mechi nyingine wa Kundi A jana Chile imeichapa Bolivia 1-0 bao pekee la mshambuliaji wa Blackburn Rovers, Benjamin Brereton dakika ya 10 Uwanja wa Pantanal, Cuiaba, Mato Grosso.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: ARGENTINA YAPATA USHINDI WA KWANZA COPA AMERICA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top