• HABARI MPYA

  Wednesday, June 16, 2021

  KAMATI YA UCHAGUZI ‘YAMCHINJA’ KAPTENI WA ZAMANI WA TAIFA STARS ALLY MAYAY TEMBELE KUGOMBEA URAIS TFF

  KAMATI ya Uchaguzi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) chini ya Mwenyekiti wake, Wakili Kiomoni Kibamba imemuengua nahodha wa zamani wa timu ya taifa, Ally Mayay Tembele kuwania Urais wa shirikisho hilo katika uchaguzi uliopangwa kufanyika Agosti 7 Jijini Tanga.
  Akisoma taarifa yake kikao cha Kamati kilichofanyika jana, Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya TFF Wakili Benjamin Kalume amesema kwamba wagombea watatu tu wamepitishwa kuwania Urais – ambao ni Rais wa sasa Wallace Karia, Hawa Mniga na Evans Mgeusa.
  Kuhusu wagombea walioenguliwa, Mayay, mwanahabari nguli, Ally Saleh wa Zanzibar na mchambuzi Oscar Oscar amesema hawakukidhi vigezo na sifa za kugombea.


  Katika uchaguzi uliofanyika Agosti 12, mwaka 2017 kwenye ukumbi wa mikutano wa jengo la St. Gasper Jijini Dodoma, Mayay aligombea nafasi na akashindwa na Karia aliyekuwa anagombea kwa mara ya kwanza Urais wa TFF.
  Karia alipata kura 95 kati ya 125 zilizopigwa, akifuatiwa na Ally Mayay aliyepata tisa sawa na mgombea mwingine, Shija Richard waliopata kura 9 kila mmoja.  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KAMATI YA UCHAGUZI ‘YAMCHINJA’ KAPTENI WA ZAMANI WA TAIFA STARS ALLY MAYAY TEMBELE KUGOMBEA URAIS TFF Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top