• HABARI MPYA

  Sunday, June 20, 2021

  YANGA SC YATUMIA DAKIKA MOJA YA MWISHO KUPATA MABAO MAWILI NA KUTOKA NYUMA KWA 2-1 NA KUSHINDA 3-2 DHIDI YA MWADUI FC DAR

  WENYEJI, Yanga SC wametoka nyuma na kushinda 3-2 dhidi ya Mwadui FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara usiku huu Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
  Mabao ya Mwadui FC yamefungwa na Aniceth Revocatus yote dakika ya saba na 42, wakati ya Yanga yamefungwa na Bakari Mwamnyeto dakika ya 22, Yacouba Sogne dakika ya 90 na Waziri Junior dakika ya 90 na ushei.
  Mshambuliaji Mrundi, Fiston Abdulrazak alikosa penalti kipindi cha kwaza baada ya Feisal Salum kuangushwa kwenye boksi ambayo ingeipa Yanga uongozi wa 2-1.


  Yanga SC inafikisha pointi 67 baada ya kucheza mechi 31, ingawa inabaki nafasi ya pili ikizidiwa pointi tatu na mabingwa watetezi, Simba SC ambao pia wana mechi tatu mkononi, wakati Mwadui ambayo imeshashuka daraja inabaki mkiani na pointi zake 19 za mechi 32.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA SC YATUMIA DAKIKA MOJA YA MWISHO KUPATA MABAO MAWILI NA KUTOKA NYUMA KWA 2-1 NA KUSHINDA 3-2 DHIDI YA MWADUI FC DAR Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top