• HABARI MPYA

  Saturday, June 19, 2021

  LUIS MIQUISSONE AFUNGA BAO PEKEE CCM KIRUMBA SIMBA SC YAICHAPA POLISI TANZANIA 1-0 JIJINI MWANZA

  MABINGWA watetezi, Simba SC wameibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya Polisi Tanzania katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza.
  Pongezi kwa mfungaji wa bao hilo pekee, kiungo mshambuliaji wa kimataifa wa Msumbiji, Luis Jose Miquissone kwa shuti la umbali wa mita 20 la mpira wa adhabu dakika ya 28 kufuatia beki wa kulia, Shomari Kapombe kuchezewa rafu nje ya boksi.
  Simba SC wanafikisha pointi 70 baada ya mechi 28 na kuendelea kuongoza Ligi Kuu kwa pointi sita zaidi sasa dhidi ya watani wao wa jadi, Yanga SC ambao pia wamecheza mechi mbili zaidi.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: LUIS MIQUISSONE AFUNGA BAO PEKEE CCM KIRUMBA SIMBA SC YAICHAPA POLISI TANZANIA 1-0 JIJINI MWANZA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top