• HABARI MPYA

  Tuesday, June 22, 2021

  SIMBA SC YAENDELEZA UBABE LIGI KUU, YAICHAPA MBEYA CITY 4-1 UWANJA WA MKAPA

   MABINGWA watetezi, Simba SC wameendeleza ubabe katika Ligi Kuu ya Tanzania Bara baada ya ushindi wa 4-1 dhidi ya Mbeya City usiku huu Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
  Mabao ya Simba SC yamefungwa na Rally Bwalya dakika ya 31, Luis Miquissone dakika ya 35, Nahodha John Bocco dakika ya 47 na Clatous Chama dakika ya 86, wakati la Mbeya City limefungwa na Pastory Athanas dakika ya 51.
  Simba SC inafikisha pointi 73 baada ya ushindi huo katika mechi ya 29 na kuendelea kuongoza Ligi Kuu kwa pointi sita zaidi ya mahasimu wao wa jadi, Yanga SC ambao pia wamecheza mechi mbili zaidi.
  Mbeya City yenyewe baada ya kupoteza mchezo wa leo katika mechi ya 32, wanabaki na pointi zao 36 katika nafasi ya 13.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA SC YAENDELEZA UBABE LIGI KUU, YAICHAPA MBEYA CITY 4-1 UWANJA WA MKAPA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top