• HABARI MPYA

  Sunday, June 13, 2021

  TAIFA STARS YANG'ARA BENJAMIN MKAPA, YAICHAPA MALAWI 2-0 MECHI YA KIRAFIKI YA KIMATAIFA MABAO YA BOCCO NA MWENDA MPISHI KIBU DENNIS

   TANZANIA imetumia vizuri Uwanja wa nyumbani, Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salam baada ya ushindi wa 2-0 dhidi ya Malawi katika mchezo wa kirafiki wa Kimataifa.
  Baada ya dakika 45 ngumu za kipindi cha kwanza, Taifa Stars ikaifungua safu ya ulinzi ya The Flames kwa mabao ya Nahodha John dakika ya 68 na Israel Patrick Mwenda dakika ya 75.
  Na mabao yote yalipikwa na mshambuliaji chipukizi wa Mbeya City, Kibu Dennis aliyetokea benchi kipindi cha pili, la kwanza akimsetia Bocco kabla ya kuangushwa nje kidogo ya boksi na Mwenda akafunga kwa shuti la mpira wa adhabu.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: TAIFA STARS YANG'ARA BENJAMIN MKAPA, YAICHAPA MALAWI 2-0 MECHI YA KIRAFIKI YA KIMATAIFA MABAO YA BOCCO NA MWENDA MPISHI KIBU DENNIS Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top