• HABARI MPYA

  Sunday, June 13, 2021

  PAN AFRICANS, GREEN WARRIORS, MASHUJAA NA DTB ZAPANDA DARAJA LA KWANZA, LIPULI YAZIDI 'KUPOTELEA MBALI'

  MABINGWA wa zamani wa Tanzania, Pan African wamefanikiwa kurejea Ligi Daraja la Kwanza katika harakati zao kuisaka Ligi Kuu.
  Pan yenye maskani yake Mtaa wa Swahili Jijini Dar es Salaam wamepanda baada ya ushindi wa jumla wa 2-0 dhidi ya Lipuli ya Iringa katika mechi mbili za mchujo.
  Pamoja na mabingwa hao wa Ligi Kuu 1982, timu nyingine zilizopanda Daraja la Kwanza kutoka la pili, nyingine Green Warriors, DTB FC za Dar es Salaam pia na Mashujaa ya Kigoma.


  Bahati mbaya kwao, Lipuli ya Iringa na AFC ya Arusha, zamani Ndovu zimeporomoka hadi Daraja la Pili baada ya mechi za mchujo.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: PAN AFRICANS, GREEN WARRIORS, MASHUJAA NA DTB ZAPANDA DARAJA LA KWANZA, LIPULI YAZIDI 'KUPOTELEA MBALI' Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top