• HABARI MPYA

  Monday, June 21, 2021

  AZAM FC YALAZIMISHWA SARE YA 0-0 NA NAMUNGO RUANGWA, KMC NA MTIBWA SUGAR WATOKA 1-1 UWANJA WA UHURU

   TIMU ya Azam FC imelazimishwa sare ya bila kufungana na Namungo FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Majaliwa, Ruangwa mkoani Lindi.
  Sare hiyo inayoiongezea kila timu pointi moja, inaifanya Azam FC ifikishe pointi 64 baada ya kucheza mechi 32 sasa, ingawa inabaki nafasi ya tatu ikizidiwa pointi tatu na Yanga ambayo pia ina mechi moja mkononi, wakati Namungo FC inafikisha pointi 43 za mechi 32 pia na inabaki nafasi ya tano,  ikizidiwa pointi sita na Biashara United.
  Mechi nyingine ya Ligi Kuu leo, KMC imelazimishwa sare ya 1-1 na Mtibwa Sugar jioni ya leo Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam, timu ya Manungu mkoani Morogoro ikitangulia kwa bao la Kelvin Sabato dakika ya 55, kabla ya wenyeji 'Watoto wa Kinondoni' kusawazisha kupitia kwa Cliff Buyoya dakika ya 82.


  KMC inafikisha pointi 42 za mechi 31 sasa katika nafasi ya tano na Mtibwa Sugar imefikisha pointi 38 baada ya kucheza mechi 32 na kusogea nafasi ya 10.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AZAM FC YALAZIMISHWA SARE YA 0-0 NA NAMUNGO RUANGWA, KMC NA MTIBWA SUGAR WATOKA 1-1 UWANJA WA UHURU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top