• HABARI MPYA

  Sunday, June 20, 2021

  MSUVA ATOKEA BENCHI NA KUSHINDWA KUINUSURU WYDAD NA KIPIGO CHA NYUMBANI KUTOKA KWA KAIZER CHIEFS CASABLANCA

   KIUNGO mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Simon Happygod Msuva ametokea benchi na kushindwa kuiepusha timu yake, Wydad Athletic na kipigo cha 1-0 nyumbani kutoka kwa Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini usiku huu Uwanja wa Mohamed V Jijini Casablanca.
  Katika mchezo huo wa kwanza wa Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika, Msuva aliingia uwanjani dakika ya 68 kuchukua nafasi ya Muaid Ellafi.
  Na bao pekee la Kaizer limefungwa na mshambuliaji Mserbia, Samir Nurkovic dakika ya 34 akimalizia pasi ya beki Mzawa, Njabulo Blom.


  Mchezo mwingine wa Nusu Fainali ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa, watetezi wa taji, Al Ahly ya Misri pia wameshinda ugenini 1-0 dhidi ya Esperance, bao pekee la Mohamed Sherif dakika ya 67 Uwanja Olympique de Radès Jijini Tunis, Tunisia.
  Mechi za marudiano zitachezwa Jumamosi ijayo Cairo na Johannesburg na washindi wa jumla watakutana kwenye fainali Julai 17.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MSUVA ATOKEA BENCHI NA KUSHINDWA KUINUSURU WYDAD NA KIPIGO CHA NYUMBANI KUTOKA KWA KAIZER CHIEFS CASABLANCA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top