• HABARI MPYA

  Friday, June 18, 2021

  NEYAMR AFUNGA TENA BRAZIL YASHINDA 4-0 COPA AMERICA

  BRAZIL imeendeleza wimbi la ushindi katika Copa America baada ya kuichapa Peru 4-0 katika mchezo wa Kundi B usiku wa kuamkia leo Uwana wa Nilton Santos Jijini Rio de Janeiro.
  Mabao ya Brazil yamefungwa na Alex Sandro dakika ya 12 akimalizia pasi ya Gabriel Jesus, Neymar dakika ya 68 pasi ya Fred, Everton Ribeiro dakika ya 89 pasi ya Richarlison ambaye alifunga bao la nne dakika ya 90 na ushei.
  Neymar sasa amefikisha jumla ya mabao 68 aliyoifungia timu ya taifa ya Brazil akiwa anashika nafasi ya pili katika orodha ya wafungaki wa muda wote, nyuma ya Pele mwenye mabao 77.
  Mechi nyingine ya kundi hilo jana, Colombia ililazimishwa sare ya bila kufungana na Venezuela Uwanja wa Olimpico Pedro Ludovico Teixeira Jijini Goiania, Goias.

  Brazil inaendelea kuongoza kundi B kwa pointi zake sita sasa, ikifuatiwa na Colombia pointi nne, Venezuela moja baada ya wote kucheza mechi mbili, wakati Ecuador na Peru zilizocheza mechi moja kila timu hazina pointi.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: NEYAMR AFUNGA TENA BRAZIL YASHINDA 4-0 COPA AMERICA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top