• HABARI MPYA

  Tuesday, June 15, 2021

  NI AZAM NA YANGA, MTIBWA SUGAR NA SIMBA SC NUSU FAINALI LIGI KUU YA VIJANA U20

   TIMU za Azam FC na Mtibwa Sugar zimefanikiwa kwenda Nusu Fainali ya Ligi ya Vijana chini ya umri wa miaka 20 baada ya kuzipiku Tanzania Prisons na Kagera Sugar kutoka Kundi B Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es Salaam.
  Mtibwa Sugar imewachapa Kagera Sugar 5-0, mabao ya Omar Marungu dakika ya saba na 61, Anderson Shirima aliyejifunga dakika ya 30, Nickson Mosha dakika ya 34 na Joseph Mkele dakika ya 48 na Azam FC ikalazimishwa sare ya bila kufungana na Tanzania Prisons.
  Mtibwa Sugar imeongoza Kundo kwa pointi zake saba, wakati Azam FC imemaliza na pointi tano katika nafasi ya pili.
  Azam FC itamenyana na vinara wa Kundi A, Yanga SC wakati Mtibwa Sugar itamenyana na washindi wa pili wa Kundi A, Simba SC katika mechi za Nusu Fainali Alhamisi hapo hapo Azam Complex.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: NI AZAM NA YANGA, MTIBWA SUGAR NA SIMBA SC NUSU FAINALI LIGI KUU YA VIJANA U20 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top