• HABARI MPYA

  Saturday, June 19, 2021

  SIMBA B YATWAA NAFASI YA TATU LIGI KUU YA VIJANA U20 BAADA YA KUIPIGA AZAM AKADEMI KWA MATUTA CHAMAZI

  TIMU ya Simba SC ilifanikiwa kumaliza nafasi ya tatu katika Ligi Kuu ya Vijana chini ya umri wa miaka 20 baada ya ushindi wa penalti 4-1 kufuatia sare ya 1-1 na wenyeji, Azam FC ndani ya dakika 90.
  Katika mchezo huo uliofanyika Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam, Wilbert John alianza kuifungia Azam Academy dakika ya tano, kabla ya Michael Joseph kuisawazishia SImba B dakika ya 19.
  Na kwenye mikwaju ya penalti ndipo Ahmed Ferusi Telu, kipa wa Simba B inayofundishwa na Nico Kiondo alipoibuka shujaa kwa kucheza mikwaju miwili ya Azam.


  Fainali ya michuano hiyo inafuatia Saa 1:00 usiku hapo hapo Azam Complex baina ya mabingwa watetezi mara mbili mfululizo, Mtibwa Sugar na Yanga SC.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA B YATWAA NAFASI YA TATU LIGI KUU YA VIJANA U20 BAADA YA KUIPIGA AZAM AKADEMI KWA MATUTA CHAMAZI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top