• HABARI MPYA

  Tuesday, June 15, 2021

  YANGA NA BIASHARA JUNI 25 TABORA, SIMBA NA AZAM JUNI 26 SONGEA KOMBE LA TFF NUSU FAINALI

  SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limetaja tarehe za mechi zs Nusu Fainali za Kombe la shirikisho hilo, maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) zitakazochezwa mwishoni mwa mwezi huu Ruvuma na Tabora.
  Nusu Fainali ya kwanza itachezwa Juni 25 Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora kati ya Biashara United na Yanga SC na ya pili itafuatia Juni 26 Uwanja wa Maji Maji mjini Songea mkoani Ruvuma baina ya Azam FC na mabingwa watetezi, Simba kuanzia Saa 9:30 Alasiri.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA NA BIASHARA JUNI 25 TABORA, SIMBA NA AZAM JUNI 26 SONGEA KOMBE LA TFF NUSU FAINALI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top