WADAU wawili wamejitokeza kuwania Urais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) dhidi ya Wallace John Karia anayeshikilia nafasi hiyo katika uchaguzi uliopangwa kufanyika Agosti 7 mwaka huu Jijini Tanga.
Hao ni Evans Mgeusa na Zahor Mohamed Hajji ambao wote wamechukua fomu leo kwa gharama ya Sh. 500,000 pamoja na Karia.
Zoezi la uchukuaji fomu linatarajiwa kuendelea hadi Jumamosi Saa 10:00 jioni makao makuu ya TFF, Uwanja wa Karume Jijini Dar es Salaam au kupitia tovuti ya shirikisho hilo.
0 comments:
Post a Comment