• HABARI MPYA

  Thursday, June 17, 2021

  UBELGIJI YATINGA 16 BORA EURO 2020 BAADA YA KUICHAPA DENMARK 2-1

   UBELGIJI imetinga Hatua ya 16 Bora Euro 2020 baada ya kuilaza Denmark 2-1 katika mchezo wa Kundi B leo Uwanja wa Parken Jijini Copenhagen.
  Mabao ya Ubelgiji leo yamefungwa na viungo wa Borussia Dortmund, Thorgan Hazard dakika ya 54 na wa Manchester City, Kevin De Bruyne dakika ya 70, wakati la Denmark limefungwa na mshambuliaji mwenye asili ya Tanzania, Yussuf Poulsen wa RB Leipzig dakika ya pili tu.
  Ubelgiji inafikisha pointi sita baada ya mechi mbili na kuendelea kuongoza Kundi B, ikifuatiwa na Urusi na Finland zenye pointi tatu kila moja, wakati Denmark ambayo imepoteza mechi zote mbili za mwanzo inashika mkia.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: UBELGIJI YATINGA 16 BORA EURO 2020 BAADA YA KUICHAPA DENMARK 2-1 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top