• HABARI MPYA

  Sunday, June 13, 2021

  YANGA B YAPANDA KILELENI KUNDI A LIGI KUU YA VIJANA U20 BAADA YA KUICHAPA JKT TANZANIA 2-0 CHAMAZI

   TIMU ya Yanga jana imeibuka na ushindi wa 2-0 dhidi ya JKT Tanzania katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vijana chini ya umri wa miaka 20 Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, nje kidogo ya Jijila Dar es Salaam.
  Katika mchezo huo wa Kundi A Hatua ya Nane Bora, mabao ya Yanga B inayofundishwa na Said Maulid 'SMG' yalifungwa na Yohana Ndushi dakika ya 58 na Abby Mikimba dakika ya 77.
  Yanga SC inafikisha pointi nne baada ya mechi mbili, kufuatia sare ya bila kufungana na watani wao wa jadi, Simba katika mchezo wa ufunguzi Alhamisi na kuongoza kundi hilo kwa wastani wa mabao.
  Simba SC baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya Mwadui FC jana, hapo hapoAzam Complex sasa ni ya pili kwa pointi zake nne pia ikizidiwa bao moja na Yanga na JKT Tanzania yenye pointi tatu inafuatia.
  Mwadui FC yenye baada ya kufungwa mechi zote mbili za kwanza inashika mkia ikiwa haina ponti kuelekea mechi yake ya mwisho dhidi ya Yanga. 
  Ligi ya Vijana U20 inatarajiwa kuendelea leo kwa mechi mbili za Kundi B; Tanzania Prisons dhidi ya Mtibwa Sugar Saa 1:00 usiku na Kagera Sugar na Azam FC Saa 3:00 usiku Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA B YAPANDA KILELENI KUNDI A LIGI KUU YA VIJANA U20 BAADA YA KUICHAPA JKT TANZANIA 2-0 CHAMAZI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top