• HABARI MPYA

  Saturday, June 05, 2021

  TAASISI YA SIMBA JAMII KUFANYA MKUTANO MKUU KESHO KWA AJENDA TATU IKIWEMO UCHAGUZI MDOGO WA KUJAZA NAFASI MBILI

  TAASISI  ya Simba Jamii Tanzania, (SJTE) inatarajia kufanya mkutano Mkuu kesho ukiwa na ajenda tatu ikiwemo mapato na matumizi pamoja na uchaguzi mdogo wa kujaza nafasi mbili za uongozi.
  Mkutano huo Mkuu umedhaminiwa na kampuni ya ulinzi ya K4S kwa kulipia gharama zote ikiwemo uchaguzi wa viongozi wa taasisi hiyo na utafanyika katika ukumbi wa Lekam Buguruni Jijini Dar es Salaam.
  Akizungumza kwa niaba ya uongozi wa Taasisi hiyo Hassan Mohamed (EBS), alisema ni Kampuni ya K4S imetoa ushirikiano mkubwa katika Mkutano wao huo  kwa kulipia gharama zote za Mkutano na Uchaguzi utakaofanyika kesho.
  "Tunaishukuru sana K4S kwa kuonyesha ushirikiano kwetu, tunaomba kila Mwanachama wa SJTE aweze kuhudhuria Mkutano wetu Mkuu, kuna mengi yanaakuja kwetu wana SJ" alisema Mohamed .       
  Mohamed alisema Kampuni ya K4S chini ya Mkurugenzi wake Mohamed Soloka, ametoa ushirikiano mkubwa wa kudhamini Mkutano huo Mkuu wa Simba Jamii.
  Alisema kuwa Mkutano huo ni wa kwanza  katika uongozi wao tangu ufanyike Uchaguzi Mkuu na utakuwa na Ajenda tatu ambazo ni mapato na matumizi ya uongozi uliopita, Ajenda ya pili ni mapato na matumizi ya uongozi wao ambao uliingia madarakani mwezi Januari 31 na kufanyika uchaguzi mdogo wa kujaza nafasi mbili za wazi kwa wajumbe wa Kamati ya Utendaji.  
  Taasisi ya Simba Jamii (SJTE) imekuwa ikijihisisha na kutoa misaada kwa watu mbalimbali wenye uhitaji (Walemavu) maalum na vituo vya watoto yatima.      Mwisho

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: TAASISI YA SIMBA JAMII KUFANYA MKUTANO MKUU KESHO KWA AJENDA TATU IKIWEMO UCHAGUZI MDOGO WA KUJAZA NAFASI MBILI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top