• HABARI MPYA

  Wednesday, June 09, 2021

  NEYMAR AFUNGA BRAZIL YAICHAPA PARAGUAY 2-0 KWAO

  BRAZIL imetanua uongozi katika mbio za Kombe la Dunia 2022 Qatar baada ya ushindi wa 2-0 dhidi ya Paraguay usiku wa kuamkia leo Uwanja wa Defensores del Chaco Jijini Asunción.
  Mabao ya Brazil yamefungwa na Neymar dakika ya nne, akimalizia pasi ya Gabriel Jesus na Lucas Paqueta dakika ya 90 na ushei, huo ukiwa ushindi wa kwanza kwa timu hiyo nchini Paraguay ndani ya miaka 35. 
  Sasa Brazil inafikisha pointi 18 baada ya kucheza mechi sita na kuendelea kuongoza mbio hizo kwa Amerika Kusini kwa pointi sita zaidi ya Argentina iliyolazimishwa sare ya 2-2 na Colombia Uwanja wa Metropolitano Roberto Melendez Jijini Barranquilla.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: NEYMAR AFUNGA BRAZIL YAICHAPA PARAGUAY 2-0 KWAO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top